TRAINING INSTITUTE

KOZI YAWAHUDUMU NDANI YA NDEGE (CABIN CREW).

Chuo Cha Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL Training Institute ) kina furaha kuwatangazia watanzania wote kuwa kitaendesha kozi ya wahudumu ndani ya ndege (Cabin Crew ) kuanzia tarehe 01/03/2021. Kozi hii ni ya muda wa miezi mitatu (03), chuo kipo uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere-Dar es salaam(JNIA) terminal one kwenye jengo la utawala ATCL karibu kabisa na kituo cha polisi uwanja wa ndege. Chuo kinakaribisha maombi ya kujiunga na kozi hii kwa wenye sifa zilizoainishwa hapo chini. Mwisho wakupokea maombi ni tarehe 04/02/2021.

  • Sifa za mwombaji.
  • Awe na umri kuanzia miaka 18 hadi miaka 25
  • Awe timamu kiakili, kimaumbile na urefu kuanzia futi 5”4 nakuendelea
  • Elimu sio chini kidato cha nne na ufaulu mzuri hasa masomo ya kiingereza, Jiografia na Historia
  • Aweze kuongea na kuandika kwa ufasaha lugha ya Kiswahili na Kiingereza. Muombaji mwenye uelewa wa lugha zaidi ya hizi mbili kama Kiarabu, Kichina, Kihindi na Kifaransa atapewa kipaumbele.
  • Awe Mtanzania au raia wa kigeni mwenye vibali halali vinavyomruhusu kukaa na kusoma nchini.

Barua ya maombi iambatane na vitu vifuatavyo:-.

  • Nakalaza vyeti vya shule/Chuo alikosoma
  • Nakala ya cheti cha kuzaliwa
  • Picha mbili ndogo (passport size) na picha moja yenye kuonesha umbo lote ukubwa wa 6x8
  • Curriculum Vitae - CV

Maombi yatumwe kwa:

 
Principal
ATCL Training Institute 
S.L.P 543 
Dar es salaam
Barua pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Mobile: +255735787212 , Landline: +255222842543
ATCL TRAINING INSTITUTE.